Februari 7, 2024 Mahakama ya Wilaya ya Lindi imemhukumu Bw. Isaya Makali Lucas,
Daktari tarajali wa Hospitali ya Rufaa Sokoine na Mkazi wa Mtaa wa Mtanda Wilaya ya Lindi, baada ya kukiri makosa na kulipa faini ya Shilingi 1,000,000/= au kwenda jela mwaka mmoja, kwa makosa ya kushawisi na kupokea hongo ya Shilingi 70,000/=.
Hukumu hiyo dhidi ya Isaya Makali Lucas katika shauri la jinai Na. 03/2024, imetolewa chini ya Mhe. Maria Batulaine – Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi Febuari 7, 2024.
Mshtakiwa huyo alipokea hongo ya Shilingi 70,000/= kutoka kwa ndugu wa mgonjwa Bw. Yusufu Hamisi Juma, ambaye alikua anamuuguza Bw. Saidi Omari Nyanyari.
Mshtakiwa amelipa faini ya TZS. 500,000/ = kwa kila kosa na kuachiwa huru.
Kesi hii imeendeshwa na waendesha mashtaka Yakubu Simba na Fatma Chimbyangu wa TAKUKURU Lindi.