Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Ushauri wa Wataalamu unaolenga kuanzisha Jukwaa la wataalam watekelezaji wa masuala ya urejeshwaji mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu – Barani Afrika –THE EXPERTS CONSULTATIVE MEETING FOR ESTABLISHMENT OF AN ASSET RECOVERY PRACTITIONERS’ FORUM FOR AFRICA . Mkutano huo uliofanyika Jijini Dar Es Salaam kwa siku tatu ulifunguliwa rasmi Januari 30, 2024 na Bibi Neema Mwakalyelye – Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu na kusema kuwa Bara la Afrika limekuwa likipoteza fedha nyingi kutokana na ubadhirifu.“According to the Report of the High Level Panel on Illicit Financial Flows from Africa (UNODC 2011) Africa is losing billions of dollars in illicit financial flows—twice as much as it receives in aid’. Alisema Naibu Mkurugenzi Mkuu.
Mkutano huu utakaohitimishwa Februari 1, 2024, umeandaliwa kwa ushirikiano wa African Union Advisory Board against Corruption; the African Union Commission – Political Affairs Peace and Security Department pamoja na GIZ Global Program on Illicit Financial Flows ambapo pamoja na TAKUKURU washiriki wengine ni wataalam wa urejeshwaji mali kutoka Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa za nchi za Umoja wa Afrika, Taasisi za Kikanda na Kimataifa pamoja na Wadau wa Maendeleo.