MHASIBU NHBRA AHUKUMIWA KWA UBADHIRIFU.
Kesi Namba Ecc 37709/2023 imeamuliwa Januari 25, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Wilaya ya Kinondoni ambapo mshtakiwa Bw. EZEKIEL SAGITII – Mhasibu katika Shirika la Wakala wa Taifa la Utafiti na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA), amehukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu (3,000,000/=) au kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) jela.
Adhabu hiyo ambayo inaenda sambamba na kurudisha fedha kiasi cha shilingi 16,990,000 kilichofanyiwa ubadhirifu, imetokana na kosa la ubadhirifu Kinyume na kifungu cha 28 Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329.
Mshtakiwa alifanya ubadhirifu wa fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha watumishi wanne wa shirika hilo kwenda katika kongamano.
Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Mheshimiwa Ishak Khuppa na mshatakiwa amelipa faini.