Januari 15, 2024 Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bibi Neema Mwakalyelye amepokea ugeni wa Wataalamu wanne wa Mradi wa BUILDING SUSTAINABLE ANTI CORRUPTION ACTION IN TANZANIA (BSAAT) kutoka Uingereza. Ugeni huu umefika TAKUKURU kwa lengo la kubaini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa shughuli zinazofadhiliwa na mradi wa BSAAT kwa Mwaka 2023.