Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU imesaini Makubaliano ya Ushirikiano wa Kikazi (MoU) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania – OUT.
MoU hii imesainiwa Desemba 19, 2023 jijini Dar Es Salaam, ikiwa na lengo la kurasimisha na kuimarisha mashirikiano yaliyopo kati ya taasisi hizi mbili