AFISA KILIMO MBARONI KWA KOSA LA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA;
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Njombe Bw RASHID MUSTAPHA MAKOCHA amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi cha sh 10,000/=.
Akisoma hukumu katika kesi hiyo Na.1/2022 Mhe Isaack Mlowe – Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa Kinyume na Kifungu cha15 (1) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 Marejeo ya 2022, kwa kumshawishi mkulima ili aweze kumsajili kwenye Daftari la Wakulima ili awe mnufaika wa Mbolea ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faini ya sh. 500,000/= au kutumikia kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kwanza na faini ya sh 500,000 au kifungo cha miaka 5 kwa kosa la pili. Pia imeamuliwa fedha ya mtego sh 10 000 irudishwe Serikalini.
TAKUKURU Njombe, Disemba15, 2023