ALIYEKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KIJIJI AHUKUMIWA KWA HONGO:
Mahakama ya Wilaya ya Liwale imemhukumu Bw. Khalidi Rashid Mingoli, aliyekuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Kikulyungu na Mkazi wa Kijiji hicho, baada ya kukiri kosa na kuamriwa kulipa faini ya Shilingi 500,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa kosa la kupokea hongo ya Shilingi 600,000/=.
Hukumu hiyo dhidi ya Khalidi Rashid Mingoli katika Shauri la Jinai Na. 1062/2024, imetolewa chini ya Mhe. Christopher Makwaya – Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Liwale Januari 15, 2024.
Mshtakiwa huyo alipokea hongo jumla ya Shilingi 600,000/= kutoka kwa wafugaji watatu waliokuwa wameingiza mifugo kwenye ardhi ya Kijiji cha Kikulyungu kinyume na utaratibu ili asiwachukulie hatua za kisheria.
Mshtakiwa amelipa faini Tshs. 500,000/ = na kuachiwa huru.
Kesi hii imeendeshwa na Wakili Salum Bhoki wa TAKUKURU Lindi.