Januari 5, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Shauri la Uhujumu Uchumi ECC. 16/2023 limetolewa maamuzi ambapo Washtakiwa watatu kati ya nane ambao ni A/Isnp. Hillary Ferdinand Komba, PC – Bartholomew Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta, wametiwa hatiani na wote kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kinyume na k/f cha 31 cha PCCA Cap 329 RE 2019.
Washtakiwa wamehukumiwa kwa kitendo cha kufika nyumbani kwa Prof. Justine Maeda na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu.
Aidha, washtakiwa watano wameachiwa huru kwa kuwa ushahidi haukuweza kuthibitisha makosa dhidi yao.
Itakumbukwa kuwa mnamo Machi 21, 2021 washtakiwa hawa walikwenda nyumbani kwa Prof. Maeda na kufanya upekuzi kinyume na utaratibu na kisha kutumia nguvu kupokea kiasi cha Tsh 73,000,000 kutoka kwa Prof Maeda ili wasimchukulie hatua za kisheria dhidi yake kwa tuhuma za uongo kuwa alikuwa akimiliki pembe za ndovu, tuhuma ambazo hazikuwa za kweli.