AFISA AFYA BUGURUNI ASHTAKIWA KWA UBADHIRIFU.
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 534/2024 – Jamhuri dhidi ya Bw. RENATUS ANATORY RWEHABURA-Afisa Afya wa Kata ya Buguruni katika Halmashauri ya Manispaa Ilala limefunguliwa Januari 10, 2024 mbele ya Mhe. Rehema Lyana (SRM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Mshtakiwa ameshtakiwa kwa kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa fedha kiasi cha Tsh. 62,292 000/= kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA 329 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, R.E 2022.
Mshtakiwa amekana kosa na kupelekwa mahabusu baada ya kutokukidhi masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Januari 24, 2024 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.