Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, mbele ya Mhe. Jaji Luvanda, Desemba 22, 2023 katika Shauri No. 10/22 imetoa hukumu kwa Washtakiwa Wanne wafuatao:
- Robert Simon Kisena Executive Chairman UDART
- Charles Selemani Newe – Group Chief Finance Manager-UDART
- JOHN Ng’wala Samangu –
Mkurugenzi wa Universal Cargo Trans Shipment Holding - Tumaini Deusdedith Kulwa – Cashier UDART
Washtakiwa hawa Walishtakiwa kwa makosa ya Kuendesha genge la Uhalifu; Kugushi; Kuwasilisha nyaraka za uwongo; Kutakatisha fedha na Kuisababishia Serikali hasara.
Katika hukumu hiyo washtakiwa namba 1, 2 & 4 wametiwa hatiani na mshtakiwa No. 3 ameachiwa huru.
Vilevile Mshtakiwa wa kwanza na wa pili wametiwa hatiani kwa makosa ya Kuendesha genge la uhalifu; Kugushi; Utakatishaji fedha na Kuisababishia Serikali hasara.
Aidha Mshtakiwa wa nne(4) ametiwa hatiani kwa makosa ya Kuendesha genge la uhalifu; Kuwasilisha nyaraka za uwongo; Kutakatisha fedha na Kuisababishia Serikali hasara.
Adhabu katika kosa la Kuendesha genge la uhalifu ni kifungo cha miaka mitano gerezani na kosa la Kugushi ni kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Pia kwa kosa la kuwasilisha nyaraka za uwongo adhabu ni kifungo cha miaka mitatu gerezani wakati kosa la Utakatishaji fedha adhabu yake ni fine ya sh. Milioni 100 au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.
Kosa la kuisababishia Serikali hasara adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu gerezani.