WAZIRI MKUU AZINDUA NACSAP IV: AWATAKA WATANZANIA KUTOKUBALI KUTOA RUSHWA

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amewataka Watanzania kutokubali kutoa rushwa mahali popote huku akisisitiza kuwa wananchi ni wadau muhimu katika mapambano dhidi ya Rushwa. “Ninyi ni wadau wakubwa wa kukomesha rushwa na ninyi ni wadau wakubwa wa kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ili nchi yetu isiwe na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi mnapaswa kufichua vitendo vya ukosefu wa maadili na uvunjifu wa haki za binadamu,” amesema Mhe. Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri Mkuu amezindua Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Nne (NACSAP IV) na kuusanbaza kwa wadau.

Mhe. Waziri Mkuu ametekeleza majukumu haya Disemba 10, 2023 wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa 2023, jijini Dodoma.

Taarifa kwa Umma