WAZIRI UTAWALA BORA AHIMIZA KUZUIA RUSHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Mhe. George Simbachawene (MB), amefungua Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Juhudi Dhidi ya Rushwa lililofanyika Jijini Dodoma Desemba 4, 2023 na kuwataka wadau walioshiriki KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA KUZUIA RUSHWA NCHINI.

Waziri Simbachawene amesema tatizo la Rushwa ni changamoto katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo hivyo washiriki wa Jukwaa waitumie fursa hiyo kujadili njia sahihi na bora zaidi za kuzuia vitendo vya rushwa badala ya kusubiri kupambana nayo. “Tutumie nguvu kubwa zaidi kuzuia vitendo vya rushwa kabla ya kutokea”, alisema Waziri Simbachawene na kutoa wito kwa Watanzania – kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika kuzuia Rushwa kama kaulimbiu ya TAKUKURU inavyosema KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU TUTIMIZE WAJIBU WETU.

Kongomano hili limefanyika ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa inayoadhimishwa Desemba 10 kila Mwaka.

Taarifa kwa Umma

KUTOKA MAHAKAMANI SONGWE