AFISA BIASHARA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA RUSHWA- NGARA
Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bi IRENE LUCAS MWAKABANGA, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ngara akishtakiwa kwa ubadhilifu wa shs 15,240,000/=
Akisoma shtaka katika kesi hiyo Na. ECC. 8/2023 mbele ya hakimu wa Mahakama hiyo Mhe. T.C. Tesha, mwendesha mashitaka wa Serikali Bw Haruna Shomari alisema kosa hilo ni kinyume na vifungu vya 28 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [Sura ya 329 Marejeo ya 2022], pamoja na Aya ya 10 ya Jedwali la Kwanza la Sheria ya Uhujumu Uchumi [Sura ya 200 Marejeo ya 2019 ].
Mshtakiwa alikana mashtaka yake na aliachiwa kwa dhamana.
Shauri hilo limeahirishwa hadi tarehe 20 Desemba 2023 ambapo mshitakiwa atasomewa hoja za awali.