Novemba 28, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Bukoba, mbele ya Mhe. KABUKA- Hakimu Mfawidhi, imeamriwa kesi ya rushwa Na. 4/2023 Jamhuri dhidi ya Denis Mashankara, ambaye ni Katibu wa Machinga – Soko la Machinjioni lililopo Kashai- Manispaa ya Bukoba.
Imemtia hatiani kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na k/f cha 15 cha PCCA Sura ya 329 kwa kushawishi na kupokea kiasi cha shilingi elfu hamsini (sh. 50,000), ili aweze kumuorodhesha Bw. Godlove Kahes kama mmoja wa machinga ili kibanda chake kisiondolewe wakati wa ujenzi wa stendi ya mabasi madogo katika Soko la Machinjioni.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 2 jela au fine ya shilingi laki tano.
Kesi iliongozwa na Wakili Daudi Jacob Oringa . TAKUKURU KAGERA, Novemba 28, 2023.