Novemba 27, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya , mbele ya Mhe. Scout Peter, imefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 38221/2023, Jamuhuri dhidi ya
Magreth Daniel Lugata ambaye ni Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania – Tawi la Mbeya.
Mshtakiwa huyo ameshtakiwa kwa kosa la kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mwajiri wake (Tanzania Red Cross Society) pamoja na kufanya ubadhirifu wa sh. 4,900,000/=.
Ilidaiwa kuwa fedha hizo aliwalipa Waratibu waliodaiwa kuhudhuria kwenye mafunzo ya ‘Covid 19 awareness and poster distribution’, huku akijua kuwa siyo kweli.
Kosa hili ni kinyume na vifungu vya 333,335 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022.
Mashtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake aliachiwa kwa dhamana na shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali (PH) Novemba 28, 2023.