Novemba 22, 2023 katika Mahakama hiyo mbele ya Mhe. KABUKA- Hakimu Mfawidhi, imeamriwa kesi ya ECO. 4/2022 Jamhuri dhidi LYDIA KOKUSHOBOKA KAOO, ambaye ni alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kashai- Munispaa ya Bukoba.
Imemtia hatiani kwa makosa mawili la kwanza matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri k/f 22 PCCA kwa kuandika barua kwa mwajiri kujifanya hajamaliza masomo ya shahada ya kwanza ndani ya muda aliopewa na mwajiri wake ili aweze kuendelea na shahada ya pili. Kosa la pili ni kuisababishia Serikali hasara k/k Aya ya 10 jedwali la kwanza EOCA kwa kuendelea kulipwa mishahara kwa kipindi cha udanganyifu asichokuwepo kazini.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 3 or fine ya 1 milioni kwa kosa la kwanza. Na kifungo cha miaka 3 bila fine kwa kosa la pili.
Pia imeamuliwa jumla ya sh. 22,252,134.73/= iliyopokelewa kama mishahara azirudishe kwa mwajiri wake.
Kesi iliongozwa na Wakili William Fussi