Novemba 21, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe Ruboroga PRM, imeamriwa kesi ya Jinai namba 161/2023, Jamhuri dhidi ya Theodosia Kumpindi aliyekuwa Mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kama Mwalimu wa Shule ya Msingi Msimbazi Mseto.
Mwalimu huyo alishtakiwa kwa kosa la Kughushi na Kujifanya mtu aliyetajwa kwenye cheti, kinyume na kifungu cha 333, 335 (d)(i), 337, 371 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2019.
Shauri tajwa lilifunguliwa tarehe 12.09.2023 na Novemba 21, 2023 mshtakiwa amekiri kutenda makosa aliyoshtakiwa kwayo, hivyo ametiwa hatiani na kuamriwa kifungo cha mwaka mmoja nje na sharti la kutokufanya kosa linaloendana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa kipindi cha mwaka mmoja (Conditional Discharge).