Novemba 22, 2023 katika Mahakama hiyo mbele ya Mhe. W. YONA SRM, imeamriwa kesi ya CC. 40/2022 Jamhuri dhidi ya THEONEST RWELAMIRA CLEMENCE ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Kasambya- Wilaya ya Miasenyi.
Imemtia hatiani kwa kosa la kutotii wajibu wa kisheria k/f 123 Penal Code kwa kushindwa kuweka kiwango cha sh. 1,632,900/= katika akaunti ya mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa H/W Missenyi alizokusanya kupitia mashine ya POS.
Kwa kuwa Mshtakiwa aliomba nafuu ya kwamba alishachukuliwa hatua za nidhamu na mwajiri wake na kutakiwa kulilipa deni lote pamoja na makato ya 15% ya mshahara wake kwa miaka mitano na hadi sasa hadaiwi chochote na pia alishapewa adhabu ya kushishwa daraja la cheo chake.
Mshtakiwa ametiwa Hatiani na kupewa kifungo cha nje kwa miezi 6 kutotenda kosa lingine lolote.
Kesi iliongozwa na Wakili William Fussi