Novemba 22, 2023 imefunguliwa kesi ya Jinai namba CC. 37862/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele mbele ya Mhe. Rioba, Jamhuri dhidi ya BENARD ZUBERI MASALA mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi.
Hati ya Mashtaka imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU John Kitutu, kwamba tarehe 13 Mwezi Novemba 2023 Mshtakiwa alifanya jaribio la kutoa kiasi cha shilingi 1,196,000/= kwa MARTIN KAYAGE ULIMBA ambaye ni Manager wa Wakala wa misitu Wilaya ya Mlele, ili ampatie eneo la hifadhi ekari 30 alime mpunga.
Mshtakiwa amejihusisha na vitendo vya Rushwa kinyume na k/f cha 15 cha sheria ya PCCA Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.
Mshtakiwa amekiri kosa, na Mahakama imemtia hatiani na kumhukumu faini ya Shilingi 500,000/= au kifungo cha miaka mitatu jela.
Sambamba na hilo Mahakama imetoa amri ya kutaifisha kiasi cha shilingi 1,196,000/= ambazo Mshtakiwa alitaka kuzitoa kama hongo.
RBC Katavi