Novemba 13, 2023 mbele ya Mhe. Fahamu Kibona limeamriwa Shauri la Uhujumu Uchumi Namba 04/2023-Jamhuri dhidi ya MELCHIORY RUTAYUGA MUKANDALA mtumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliyeshtakiwa Januari 2023, kwa kosa la kughushi nyaraka kinyume na Kanuni ya Adhabu na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Hassan Dunia ambapo baada ya Mahakama kusikiliza pande zote iliridhika kutendwa kwa kosa na kumtia hatiani mshtakiwa.
Mahakama imemhukumu mshtakiwa adhabu ya kulipa faini ya sh. Milioni moja kwa kila kosa au kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kila kosa na adhabu zote zinaenda kwa pamoja.