MAHAKAMA YA WILAYA YA KYERWA – KAGERA YAMHUKUMU MFANYABIASHARA KWA UDANGANYIFU


Novemba 10, 2023 katika Mahakama hiyo mbele ya Mhe Kubingwa Hakimu Mfawidhi Wilaya, imeamriwa kesi na CC. 97/2023 Jamhuri dhidi ya JACKSON KALIKAWE, kwa kumtia hatiani kwa makosa mawili ya kuwasilisha nyaraka iliyobeba taarifa za uongo k/f 342 Penal Code.

Kwamba mshtakiwa alitumia nyaraka ambazo ni vibali vya kusafirishia kahawa huku vikiwa kughushiwa na kubadilishwa tarehe ya mwisho wa matumizi yake.

Kesi iliongozwa na Wakili William Fussi

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya sh. 500,000/= kwa kila kosa au kwenda jela miaka 7.

Mshtakiwa amelipa faini ya sh. 1,000,000 kwa makosa yote mawili.

Taarifa kwa Umma