Oktoba 25, 2023, katika Mahakama ya Wilaya Karagwe mbele ya Mhe Florah Haule Hakimu Mfawidhi Wilaya, imeamriwa kesi Ecc. 12/2022 Jamhuri dhidi ya Viongozi watatu waliokuwa waajiriwa wa Chama cha Ushirika Karagwe mkoani Kagera.
Washtakiwa hao ni: –
- Caisalius Mathias Rugemalira – Kaimu Meneja wa KDCU;
- Renatus Gerald pamoja – Kaimu Mhasibu wa KDCU pamoja na
- Revelian M. Makune – Mwenyekiti wa Bodi ya KDCU .
Pamoja na makosa mengine ya ubadhirifu, washtakiwa hawa walishtakiwa kwa kosa la wizi wa fedha za Chama cha Ushirika Karagwe (KDCU) kiasi cha Shilingi Milioni Arobaini, Kinyume na kif cha 258 na 265 cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022.
Kesi hii iliongozwa na Wakili Kelvin Murusuri wa TAKUKURU ambapo washtakiwa wameamriwa kurejesha kiasi chote cha fedha kilichoibiwa (40,000,000/-) pamoja na kulipa faini ya sh. Milioni Moja na Laki nane (1,800,000/-) au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.