Oktoba 25, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Mbarali, mbele ya Mhe. Emily Mwambapa, imefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na 33/2023, Jamuhuri dhidi ya
Patrick Mpagama ambaye ni Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Mshitakiwa huyo ameshtakiwa kwa kosa la ubadhirifu wa kiasi cha Sh. 445,000/= mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Ilidaiwa kuwa alikusanya fedha za Ushuru wa Mazao na hakuziwasilisha na badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.
Kosa hili ni kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.
Mashtakiwa baada ya kusomewa mshtaka yake aliachiwa kwa dhamana na shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali (PH) Novemba 15, 2023.