Kesi ya jinai namba CC.246/2023 imefunguliwa Oktoba 25, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni, mbele ya Mhe. Ramadhani Rugemalila.
Mshtakiwa ni Bi. HAWA ISMAIL KIRUMBI– Mfanyabiashara na mkazi wa Segerea Jijini Dar es Salaam ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kutoa hongo ya sh.10,000,000/= kwa Askari Polisi kama kishawishi ili aweze kumsaidia shemeji yake aliyekuwa amekamatwa kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kosa hilo ni kinyume na vifungu vya 15(1)(b) & (2) vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Rejeo la 2022.
Mshtakiwa amekana shtaka na kudhaminiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 16, 2023 itakapokuja kwa ajili ya usikilizaji wa hoja za awali (PH).