Oktoba 27, 2023, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amepokea ugeni wa wajumbe wawili kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) – Bw. Chelaus Rutachururwa na Bi. Marta Spinella. Wageni hawa wako nchini kwa lengo la kutembelea na kufanya vikao kazi na Taasisi za Serikali (Ikiwemo TAKUKURU), ili kufahamu hali ya utekelezaji wa mikakati na mipango inayotekelezwa kati ya IMF na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza na wageni hawa Mkurugenzi Mkuu ameeleza mafanikio ambayo TAKUKURU imeyapata kwa kipindi cha 2022 – 2023 katika kazi za Uzuiaji Rushwa, Uchunguzi, Uendeshaji wa Mashtaka pamoja na Ushirikiano na Wadau ambapo IMF wameipongeza TAKUKURU kwa jitihada hizo.