Shauri la Jinai namba 386/2023 – Jamhuri dhidi ya Bw. Ahmed Waziri Msika, Bw. Mohammed Mohammed Magwila, Bw. Humphrey Mwakalinga na Bi. Kisura Byakuzana ambao ni wajumbe wa Kamati ya Urasimishaji Makazi Mtaa wa Kipunguni A” Kata ya Kipawa, imefunguliwa leo Oktoba 18, 2023 mbele ya Mhe. Glory Nkwera (RM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa sh.10,000,000/= (Millioni Kumi tu) kinyume na kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, R.E 2022.
Washtakiwa wamekana makosa yote 25 na kupelekwa mahabusu baada ya kutokukidhi masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi tarehe 02.11.2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.