Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amefungua Mafunzo ya Kati ya Uchunguzi kwa Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU na kuwataka kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya Taasisi. Akizungumza katika hotuba yake amesema mafunzo yanayotolewa yanalenga kuwaandaa kuwa viongozi hivyo anatarajia kuona mabadiliko katika utendaji kazi. “Baada ya mafunzo haya tunatarajia kuona ni kwa namna gani mtatusaidia kuifikia Dira ya TAKUKURU ya kuwa na TANZANIA ISIYO NA RUSHWA”. Mafunzo haya yanafanyika kwa muda wa wiki 8 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere – Kibaha na yanajumuisha Maafisa Waandamizi 100 kutoka Makao Makuu, ofisini za mikoa na wilaya . Oktoba 17, 2023.