Oktoba 18, 2023, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania – TET Dkt Aneth Komba, wamesaini MoU ya kushirikiana kuzuia Rushwa kwa kujumuisha elimu ya maadili na mapambano dhidi ya Rushwa katika Mitaala ya Shule za Msingi, Sekondari pamoja na Taasisi za Elimu.