Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 22/2023-Jamhuri dhidi ya 1.YAHYA AMOUR OMAR, 2. AUDIFASY ANGELUS MYONGA ambao ni Maafisa Ugavi katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na 3. SHANA WILLIAM MUNISI -Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kampuni ya S. Scientific Centre Limited, limefunguliwa leo tarehe 18/10/2023 mbele ya Mhe. ANNETH NYENYEMA (RM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa matano yakiwemo; Ubadhirifu na Ufujaji, Matumizi mabaya ya Mamlaka, Kughushi nyaraka, Kuwasilisha nyaraka za uongo na Kuisababishia Serikali hasara kiasi cha sh.40,362,250/=
Washtakiwa wote wamekana makosa ambapo mshtakiwa Yahya Amour na Audifasy Myonga wamepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi tarehe 1/11/2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.