Shauri la Uhujumu Uchumi namba 18/2023 – Jamhuri dhidi ya Jackson Moses Ngalama – Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa – TALGWU, Emmanuel Gilbert Mdoe – Mhasibu TALGWU, Pamela Miguna Sellemia – Mkuu wa IDARA ya mikopo TALGWU, Timothy Peter Mashishanga – Dereva imefunguliwa Oktoba 16, 2023 mbele ya Mhe. Anneth Nyenyema (RM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22; Ubadhirifu na Ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1); kusaidia kutenda kosa kinyume na kifungu cha 30 vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi. Kosa jingine ni la Utakatishaji wa fedha sh. 64,157,000/= kinyume na kifungu cha 12(d) na 13(1)(a) cha Anti Money Laundering Act 2022 .
Washtakiwa wamekana makosa yote na kupelekwa mahabusu kwa sababu kosa la utakatishaji wa fedha halina dhamana.
Kesi hii imeahirishwa hadi Oktoba 25, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.
MASHTAKA MENGINE DHIDI YA VIONGOZI WA TALGWU
Shauri la Jinai namba 384/2023 – Jamhuri dhidi ya Jackson Moses Ngalama – Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa – TALGWU; Emmanuel Gilbert Mdoe – Mhasibu TALGWU na Pamela Miguna Sellemia – Mkuu wa Idara ya Mikopo TALGWU, imefunguliwa Oktoba 16, 2023 mbele ya Mhe. Nestory Baro (PRM) katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa yakiwemo; Ubadhirifu na Ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 na kosa la Utakatishaji wa sh. 51,000,000/= kinyume na kifungu cha 12(d) na 13(1)(a) cha Anti Money Laundering Act 2022.
Washtakiwa wamekana makosa yote na kupelekwa mahabusu kwasababu kosa la Utakatishaji halina dhamana na kesi hii imeahirishwa hadi tarehe 25.10.2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali