Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni anashiriki Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC. Warsha hii ya siku 4 imefunguliwa Oktoba 11, 2023 jijini Swakopmund, Namibia na itahitimishwa Oktoba 14, 2023, lengo likiwa ni kujadili utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC wa Mwaka 2023 – 2027. Vilevile kupitia warsha hii nchi wanachama watawasilisha uzoefu wa jinsi wanavyopambana na Fedha Haramu (Illicit Financial Flows) pamoja na uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka (Trans National Organized Crime) ambapo Mkurugenzi Mkuu atawasilisha uzoefu wa Tanzania katika masuala hayo. Swakopmund – Namibia. Oktoba 11, 2023.