Kampeni hiyo inalenga kutokomeza rushwa na madawa ya kulevya kupitia klabu za wapinga rushwa na madawa ya kulevya mashuleni na vyuoni kwa nchi nzima. Pia itawafikia vijana ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa elimu. Pichani kulia ni CP. Salum Rashid Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na kulia kwake ni Kamishna Jenerali Aretas James Lyimo, Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya (DCEA) wakati wa uzinduzi huo Oktoba 4, 2023 jijini Dodoma.