Septemba 29, 2023 Mahakama ya Wilaya Kondoa mkoani Dodoma, imetoa hukumu katika Kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 8/2022, iliyokuwa ikiwakabili washtakiwa watatu wafuatao:-
- ALLY HUSSEIN MRUMA – aliyekuwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kondoa;
- IBRAHIM PETER LUENA – Meneja wa Kampuni ya ENGINEERING Plus (T) LTD pamoja na
- CHARLES MAKOBA – ambaye ni Site supervisor.
Washtakiwa wote walishtakiwa kwa makosa manne yakiwemo makosa matatu ya kutumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kinyume na k/f cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, Marejeo ya Mwaka 2022 na kosa la nne lilikuwa ni kuisababishia Serikali hasara.
Washtakiwa walijenga Mradi wa Maji wa Kijiji cha Goima Kondoa chini ya kiwango, kitendo kilichosababisha mabomba kupasuka na wananchi kukosa huduma ya maji.
Washtakiwa wote wamekutwa na hatia na wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 5 kwa mshtakiwa wa kwanza, sh. milioni 3 kwa mshtakiwa wa pili na sh. Milioni 2 kwa mshtakiwa wa tatu.