Septemba 26, 2023, Mahakama ya Wilaya Kondoa, kupitia Hakimu Mwandamizi FEISAL KAHAMBA, amewahukumu washtakiwa sita ambao ni
1.BASHIRU HASSANI DINA aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Madege
- MUTAPHA ISSA NJORO Mjumbe wa Serikali ya Kijiji
- OMARI ABDALLAH MAFITA Mjumbe wa Serikali ya Kijiji
- KASIM HASSANI MSENGI – Mjumbe wa Serikali ya Kijiji
- MAJID ISSA NJORO – Mjumbe wa Serikali ya Kijiji pamoja na
- ABDALA IDD ABDALA
Mtendaji wa Kijiji cha Madege.
Wamehukumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na k/f cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2022 na kukisababisha Kijiji hasara.
Washtakiwa waliuza shamba la Kijiji kwa sh milioni 2 bila ya kufuata utaratibu.
Kila mshtakiwa amehukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya sh milioni 2 kila mmoja.