Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. James Willbert Kaji amewapongeza Watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga kwa kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Tanga. Mhe. Kaji amepongeza kasi ya utendaji katika ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na ameahidi ushirikiano wakati wote ili kuleta ufanisi katika uzuiaji rushwa. TAKUKURU (M) Tanga Septemba 22, 2023.