Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 17/2023 – Jamhuri dhidi ya: –
- Jackson Moses Ngalama – Mkurugenzi Mtendaji wa TALGWU SUPPORT LTD;
- Emmanuel Gilbert Mdoe – Mhasibu Mkuu wa TALGWU SUPPORT LTD na
- Timothy Peter Mashishanga – Dereva wa kujitegemea, limefunguliwa Septemba 12, 2023 mbele ya Mhe. Nestory Baro – Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.
Washtakiwa wameshtakiwa kwa makosa yakiwemo; Matumizi mabaya ya madaraka; Kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri; Ubadhirifu pamoja na Ufujaji wa kiasi cha shilingi 114, 457,100 mali ya Chama cha Kusaidiana chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa (TALGWU SUPPORT LTD), makosa ambayo ni kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Washtakiwa wamekana Mashtaka na kupelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.
Kesi hii imeahirishwa hadi Septemba 18, 2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.