Bw. APOLLO ELIAS LAISER ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Makete mkoani Njombe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Makete Septemba11, 2023 na kufunguliwa Shauri Na. 27/2023 kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya shilingi 1,000,000/=, kinyume na kifungu cha 15(1),(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Kesi hii imefunguliwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Makete Mhe. DENIS RWERAMILA MUJWAHUZI ambapo Mshatakiwa anashtakiwa kwa kuomba Rushwa kutoka kwa Mwananchi mmoja (Dereva) – FREDAY HENRICK MLIGO ili aweze kuliachia gari lake lililokuwa na Kesi nyingine mahakamani hapo. Kesi hiyo nyingine ilifunguliwa na Jeshi la Uhamiaji baada ya gari hilo kukutwa na Wahamiaji haramu kutoka Ethiopia.
Mshtakiwa amekana kosa na yupo nje kwa dhamana hadi Septemba 22, 2023 Kesi hiyo itakaposikilizwa.