Mahakama ya Wilaya ya Missenyi imemhukumu Bw. Abdulnuru Muhamadi Ndyanabo, mfanyabiashara na mkazi wa Missenyi kulipa faini ya Shilingi 2,000,000 au kwenda jela miaka mitatu, kwa makosa ya kushawishi na kutoa hongo ya Shilingi 102,000/=.
Hukumu hiyo dhidi ya Abdulnuru Muhamadi Ndyanabo
katika shauri la jinai Na. 04/2023, imetolewa chini ya Mhe. Yohana Mayombya – Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Missenyi Septemba 5, 2023.
Mshtakiwa huyo alishawishi na kutoa hongo ya Shilingi 102,000/= kwa Katibu wa Baraza la Ardhi la Kata ya Msheshe wilayani Missenyi ili apatiwe upendeleo kwenye shauri la ardhi lililokuwa likisikilizwa katika baraza hilo.
Mshtakiwa amelipa faini na kuachiwa huru.