WATUMISHI TFS HATIANI KWA HONGO, WALIPA FAINI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewahukumu watumishi wawili wa Wakala wa
Misitu Tanzania (TFS), kulipa faini ya Shilingi 200,000 au kwenda jela
miaka mitatu kila mmoja kwa kosa la kupokea hongo ya Shilingi 150,000.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Damson Keya Mwansanga na Bw. Yasin Shaban Yasin
katika shauri la jinai Na. 224/2022, imetolewa leo Septemba 4, 2023.

Washtakiwa hao walifikishwa kizimbani kwa shtaka la kupokea hongo ya Shilingi 150,000 kutoka kwa mwananchi mmoja ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumkamata kwa kosa la kukata na kutumia miti ya msitu wa Hifadhi ya Loleza ya jijini Mbeya.

Washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru.

Taarifa kwa Umma

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU ATEMBELEA OFISI YA TAKUKURU MKOA WA MANYARA