Agosti 30, 2023, katika Mahakama ya Wilaya ya TABORA Mbele ya Mh. Nyakunga katika kesi ya Corruption No. 01/2023 kati ya Jamhuri dhidi ya DENIS KANTANGA MAGANGA (Ex – Police Constable), kesi ilikuja kwa kusoma hoja za awali ambapo Mwendesha Mashtaka Mwanaidi Mbuguni, alimkumbusha mshtakiwa mashitaka yake.
Baada ya hati ya mashitaka kusomwa mshitakiwa alikiri makosa yake yote na ndipo Mahakama ilitoa adhabu ya kifungo cha miaka miwili (02) jela au faini ya kiasi cha sh. laki tano (Tzs.500,000) kwa kila kosa.
Mshtakiwa alikuwa akishitakiwa kwa makosa mawili ikiwa ni kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 18,000,000 kinyume na k/f 15(1)(a) na (b) cha PCCA no. 11/2007, ili amsaidie mwananchi aliyekuwa akituhumiwa kwa kesi ya mauaji.
Mshitakiwa alilipa faini ya makosa yote mawili ambayo ilikuwa kiasi cha Tzs.1,000,000/= na kuachiwa huru.
Shs 18,000,000 alizopokea kama rushwa nayo amerejesha.