Agosti 25, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbarali , yamefunguliwa mashauri matatu ambayo ni:-
- Shauri la uhujumu uchumi Eco 24/2023 dhidi ya washitakiwa ASANTE BATWEL MWILAPWA, STANFORD ALINANUSWE BUKUKU na AFRICA MATHIAS MWAMBOGO ambao ni wakusanya ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Washitakiwa hawa wanashitakiwa kwa makosa ya Kumiliki Kifaa Haramu kwa Nia ya Kufanya Uhalifu kinyume na kifungu cha 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao pamoja na kosa la Kuisababishia Hasara Serikali.
Makosa haya waliyafanya baada ya kutengeneza mfumo wa kutengeneza risiti bandia za makusanyo ya ushuru wa mazao kitendo kilichopelekea kusababisha hasara ya shilingi 296,000/=.
Washtakiwa hawa baada ya kusomewa mashtaka, wamekana mashtaka yao na wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
- Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 25/2023 dhidi ya mshtakiwa NDUNDU HITILA MWANZENJE ambaye ni Mkusanya Ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Mshtakiwa huyu anashtakiwa kwa makosa ya Kumiliki Kifaa Haramu kwa Nia ya Kufanya Uhalifu kinyume na kifungu cha 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao pamoja na kosa la Kuisababishia Hasara Serikali.
Makosa haya aliyafanya baada ya kutengeneza mfumo wa kutengeneza risiti bandia za makusanyo ya ushuru wa mazao kitendo kilichopelekea kusababisha hasara ya shilingi 696,000/=.
Mshtakiwa huyu baada ya kusomewa mashtaka amekana mashtaka yake na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
- Shauri la Eco 26/2023 dhidi ya washitakiwa ELIA FESTO KIWALE na LUI RASHIDI GODIGODI ambao ni wakusanya ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Washtakiwa hawa wanashtakiwa kwa makosa ya Kumiliki Kifaa Haramu kwa Nia ya Kufanya Uhalifu kinyume na kifungu cha 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao pamoja na kosa la Kuisababishia Hasara Serikali.
Makosa haya waliyafanya baada ya kutengeneza mfumo wa kutengeneza risiti bandia za makusanyo ya ushuru wa mazao kitendo kilichopelekea kusababisha hasara ya shilingi 154,000/=.
Washtakiwa hawa baada ya kusomewa mashitaka wamekana mashitaka yao na wamefanikiwa kupata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Mashauri haya yamepangwa kutajwa tarehe 07/09/2023.