Agosti 31, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Kilwa, zimefunguliwa kesi mbili za Jinai kama ifuatavyo:-
- Kesi ya Jinai Namba 94/2023, Jamhuri dhidi ya SAID AKILI MTURENI – Karani wa Tawi la Naungo ‘A’ la Nanjirinji AMCOS.
- Kesi ya Jinai Namba 95/2023, Jamhuri dhidi ya AFAI RAJAB MBWANI – Karani wa Tawi la Mawelenje la Nanjirinji AMCOS.
Washitakiwa wote wanakabiliwa na makosa mawili kila mmoja kwa mujibu wa hati zao za mashtaka ambayo ni Wizi wa kuaminika K/f cha 273(b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2019 na Kughushi K/f cha 333,335(d) na 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2019.
Washitakiwa wote wawili katika kosa la kwanza wanashtakiwa kwa kuiba ufuta uliopelekwa na wakulima kwenye matawi yao: Mshtakiwa SAID AKILI MTURENI (Kilogramu 1,250 sawa na kiasi cha Tshs. 3,016,250/=) na AFAI RAJAB MBWANI (Kilogramu 2,005 za ufuta sawa na Tshs. 4,838,065/=).
Kwa kosa la pili kila mmoja anashtakiwa kughushi saini ya Mjumbe wa Bodi aliyekuwa anafanya naye kazi katika tawi lake kwenye Stakabadhi za mazao zinazoonesha kupokelewa kwa ufuta huo.
Washitakiwa wote wameshindwa kukamilisha masharti ya dhamana na Mahakama imeamuru wapelekwe Mahabusu.
Kesi hizi zitakuja Mahakamani tarehe 11/09/2023 kwa ajili ya kusomwa Hoja za Awali.