MAFUNZO YA MFUMO WA UNUNUZI WA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amepokea ugeni wa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Eliakim Maswi aliyeongozana na maafisa kutoka mamlaka hiyo katika ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma.

Ugeni huu umefika kwa lengo la kutoa mafunzo kwa Menejimenti ya TAKUKURU kuhusu ‘Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao’. Mafunzo haya ya siku moja yamefanyika Agosti 24, 2023.