Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini – TFF, watazindua rasmi Kampeni ya Kupinga Upangaji wa Matokeo. Uzinduzi huu utafanyika jioni ya Jumapili – Agosti 13, 2023 katika Viwanja vya Mpira wa Miguu – Mkwakwani jijini Tanga wakati wa Mechi ya Fainali ya Ngao ya Jamii. Bi. Sabina Seja, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa TAKUKURU, yupo jijini Tanga kushuhudia tukio hili akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu. TAKUKURU TANGA, Agosti 13, 2023.