Mhe. Waziri amewataka watumishi waitendee haki Serikali kwa kuhakikisha wanawaelimisha watumishi wa Taasisi mbalimbali kuhusu makosa yanatotamkwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ikiwa ni pamoja na kuwajulisha taratibu wanazoweza kuzifuata ili kuzuia vitendo vya rushwa katika maeneo yao. Pia ameelekeza wajikite zaidi kufuatilia Rushwa kwenye maeneo ya utoaji wa huduma za kijamii, wafanye kazi kwa bidiii na wazingatie maadili ya viapo vyao. TAKUKURU MWANZA, Agosti 4, 2023.