Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika picha ya pamoja na Wahitimu mara baada ya kumalizika kwa Mahafali ya Kozi ya 11 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) yaliofanyika katika chuo hicho kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam Julai 29, 2023. Mmoja wa wahitimu hao ni Bw. Thobias Ndaro – Mkurugenzi Msaidizi – Ufuatiliaji na Tathmini, aliyesimama mstari wa katikati – wa tatu kutoka kulia.