Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye ameshiriki Mkutano wa 25 wa kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC, uliofanyika Jijini Windhoek Namibia.
Mkutano huo ulioanza Julai 17, 2023 umehitimishwa Julai 21, 2023 huku ukikutanisha nchi wanachama wa SADC kwa ajili ya kujadili na kutathmini hali ya Siasa, Ulinzi, Usalama, Demokrasia na Utawala Bora kwa maslahi mapana ya nchi wanachama. Kiongozi wa washiriki kutoka Tanzania alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax.