Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Afrika si kichaka cha Walarushwa.
“Walarushwa wafahamu kwamba nchi za Afrika si kichaka cha kuficha fedha zilizotokana na rushwa au kufuga wala rushwa. Tunataka dunia nzima ifahamu kuwa, Afrika si salama kwa walarushwa na hilo lionekane kwa kupitia vitendo vyetu dhidi ya rushwa”.Rais Samia ameyasema hayo Julai 11, 2023 alipokuwa akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyoadhimishwa Jijini Arusha Julai 9 – 11, 2023.
Maadhimisho haya yalifanyika sambamba na miaka 20 ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Mwaka 2023.