Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amepokea ugeni wa Mkurugenzi wa Idara Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, ofisini kwake PCCB HOUSE Dar es Salaam. Bw. Msigwa amefika TAKUKURU kwa ajili ya mazungumzo ya kikazi. TAKUKURU Ilala – Dar es Salaam, Julai 5, 2023.