Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, amefungua mafunzo ya Viongozi wa TAKUKURU ya kutumia Mfumo wa Hesabu Serikalini – MUSE. Mfumo huu ambao utaanza kutumiwa na TAKUKURU katika mwaka huu wa fedha 2023/2024, unalenga kurahisisha na kuharakisha utaratibu wa uhasibu ndani ya Taasisi. Wawezeshaji wa mafunzo haya ni Viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Fedha. TAKUKURU Ilala – Dar es Salaam, Julai 5, 2023.